Trump ashikiliwa jela na kupigwa picha kama mhalifu na polisi

 

Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump, amejisalimisha kwenye gereza la wahalifu hatari la Kaunti ya Fulton huko Atlanta, Georgia, na kuchukuliwa picha kama mhalifu kwa mara ya kwanza.

Trump anakabiliwa na mashtaka 18 yanayohusiana na kula nyama za kutaka kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2020 katika jimbo la Georgia.

Trump analazimika kulipa dhamana ya dola laki mbili, ili kuachiliwa kwenye gereza hilo la Atlanta, wakati akingojea kesi yake kuanza kusikilizwa.

Hii ni mara ya nne kwa rais huyo wa zamani wa Marekani kukamatwa ndani ya miezi mitano kwa kesi za uhalifu, ila ni mara ya kwanza kwa polisi kumpiga picha rasmi kama mtuhumiwa wa uhalifu.

CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni