Rais wa Soka wa Hispania kuadhibiwa na FIFA kwa kumbusu mchezaji

 

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), limeanza mchakato wa kumchukulia hatua za kinidhamu Rais wa Soka wa Hispania Luis Rubiales kutoka na utovu wa nidhamu aliouonyesha kwenye fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake.

Rais huyo wa Soka wa Hispania Rubiales alifanya kitendo cha kumbusu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania, Jenni Hermoso, baada ya Hispania kushiinda Uingereza, kwenye mchezo wa fainali.

Kama hiyo haitoshi Rubiales awali alionyesha kitendo kisicho cha nidhamu cha kushika uume wake huku akishangilia ushindi, baada ya refa kupuliza kipenga cha kumaliza mchezo huyo wa fainali za Kombe la Dunia la Wanawake.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania Rubiales anatarajiwa kutangaza kujiuzulu wadhifa wa Rais wa Soka la Hispania leo Ijumaa, na tayari ameshawataarifu wenzake katika shirikisho hilo kuhusiana na uamuzi wake huo.

Chapisha Maoni

0 Maoni