Serikali ya Somalia imetangaza kupiga marufuku mitandao ya
jamii ya TikTok, Telegram pamoja na mchezo wa kubashiri mtandaoni, ikisema
mitandao hiyo inatumiwa kusambaza propaganda za magaidi.
Hatua hiyo imekuja, wakati ambapo inajiandaa na awamu ya
pili ya oparesheni ya kijeshi dhidi ya kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa
Al-Shabaab, ambalo limekuwa likifanya mauaji na kukabiliana na serikali kwa
miaka 15 sasa.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa jana, Wizara ya Teknolojia
na Mawasiliano ya Somalia imewaagiza watoa huduma za intaneti kutekeleza katazo
hilo ifikapo Agosti 24, la sivyo watakabiliana na hatua za kisheria ambazo
hazijaelezwa.
CHANZO: Nation
0 Maoni