Aliyeifungia Hispania aambiwa baba yake amekufa baada ya mchezo

 

Kapteni wa Hispania Olga Carmon, aliyeifungia nchi yake goli lililoipa Kombe la Dunia la Wanawake nchi yake, aliambiwa kuwa baba yake amekufa baada ya mchezo huo.

Carmona, mwenye umri wa miaka 23 alifunga goli pekee dhidi ya Uingereza katika mchezo wa fainali uliochezwa Jijini Sydney nchini Australia, na kutwaa kombe hilo.

Baba wa mchezaji huyo anayechezea nafasi ya beki wa kushoto kwenye timu ya Real Madrid, alikuwa anaugua kwa muda mrefu na alifariki dunia siku ya Ijumaa.

Chapisha Maoni

0 Maoni