Timu ya taifa ya wanawake ya Hispania imeifunga Uingereza na
kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la Wanawake katika mchezo wa fainali
uliochezwa Jijini Sydney nchini Australia.
Katika mchezo huo Hispania ilipata goli pekee kupitia kwa Kapteni
Olga Carmona kwa kumpita kipa Mary Earps katika kipindi cha kwanza baada ya
Lucy Bronze kupoteza mpira.
Kwa matokeo hayo Uingereza inaendelea kungojea kwa hamu
kutwa Kombe la Dunia, baada ya Hispania kuwazidi mbinu.
Simba hao wakike walionekana kuwa watakuwa timu ya kwanza ya
wakubwa ya Uingereza kutwaa ubingwa wa dunia, tangu timu ya wanaume kutwaa
kombe la dunia mwaka 1966.
Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania wakishangilia kwa kuwa mabingwa wa dunia wa Kombe la Dunia la Wanawake 2023.
0 Maoni