Harry Kane aanza Bundesliga kwa kucheka na nyavu

 

Kapteni wa England Harry Kane, amefunga na kutengeneza goli katika mchezo wake wa kwanza Bundesliga wakati mabingwa Bayern Munich wakishinda magoli 4-0 dhidi ya Werder Bremen.

Kane alitupia goli hilo wavuni kwa mpira wa chini wa shuti la guu la kulia uliompita kipa Jiri Pavlenka na kuifanya Bayern kuongoza kwa magoli mawili.

Awali Kane alitoa pande la goli lililofungwa na Leroy Sane ambaye katika mchezo huo aliifungia Bayern Munich magoli mawili.

Mchezaji Mathys Tel alikamilisha ushindi huo murua kwa kocha Thomas Tuchel katika dakika za mwishoni.

Chapisha Maoni

0 Maoni