Mkuu wa wilaya ya Kwimba, Bw. Ng’wilabuzu Ludigija, amewataka
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule za sekondari zilizopo katika wilaya
hiyo kuripoti katika shule zao, ili waanze kupata elimu baada ya serikali
kukamilisha ujenzi wa maiundombinu ya madarasa, vyoo na mabweni.
Bw. Ludigija amesema nafasi zao zipo na kama kuna wengine
wanataka kuhamia katika shule hizo za Mwamashimba, Sumve, Talo na Ngudu
wanakaribishwa huku akimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za
kuboresha na kujenga miundombinu katika shule hizo ili wanafunzi wapate
mazingira mazuri ya kujisomea.
Mkuu wa wilaya huyo amesema tangu shule zilipofunguliwa hadi
leo hii wanafunzi wanaendelea kuripoti na kwamba ataendelea kutembelea shule
hizo ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti na kuanaza masomo yao.
“Naendelea kusema kwa wananchi hasa wazazi waendelee
kuwaleta shuleni watoto wao, na shule zote za kidato cha tano tumejipanga kwa
miundombinu ya kutosha waje tu hapa tunawasubiri na vitanda vipo vya kutosha
hadi vinabaki, Rais Samia amefanya mapinduzi makubwa sana kwenye miundombinu ya
kujifunzia pamoja na madarasa na shule za kwimba ni moja kati ya shule
zinanofanya vizuri sana,” alisema Bw. Ludigija.
Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya sekondari Mwamashimba
akiwemo Hamisa Saidi na Ana Ayoub, wamemuahidi mkuu huyo wa wilaya kufanya
vizuri katika masomo yao ili warudishe fadhila kwa Rais Samia Suluhu Haasan kwa
jinsi alivyowawekea mazingira mazuri ya kujisomea.
“‘Tunapenda kumshikuru sana Rais Samia kwa kutusaidia
tulipofika hapa shuleni tukaona madarasa mabweni na vyoo vizuri tunamuahidi
kufaulu vizuri sana na tutapata division one nyingi sana tunamshukuru sana,”
walisema wanafunzi hao.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano waliochaguliwa kujiunga na shule za sekondari zilizopo katika wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza wakiwasili shuleni na mizigo yao tayari wa ajili ya kuanza masomo yao rasmi.
0 Maoni