Aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo Tanganyika na Zanzibar afariki

 

Mmoja wa miongoni mwa walioshiriki kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, Bi. Khadija Abbas Rashid, 74, amefariki dunia jana Agosti 22, 2023 nyumbani kwake Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, imethibitisha taarifa za kutokea kwa kifo cha Bi. Khadija Abbas Rashid, kupitia taarifa yao waliyoisambaza kupitia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii leo Agosti 23, 2023

Marehemu Bi. Khadija Abbas Rashid alihusika katika tukio hilo la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. 


Chapisha Maoni

0 Maoni