Wavulana waongoza ufaulu matokeo kidato cha sita

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023, ambayo yameonyesha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka jana.

Akitangaza matokeo hayo leo huko Zanzibar, Katibu Mtendaji wa Necta Dkt. Said Mohamed ameeleza jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani ni 106, 883 huku wasichana wakiwa 47, 340 na wavulana 59, 543.

Matokeohayo yanaonyesha kuwa aasichana waliofaulu ni 46,707 sawa na asilimia 99.51  huku kwa upande wa wavulana, waliofaulu ni 57, 843 sawa na asilimia 99.

Angalia matokeo yote ya kidato cha sita kwa kubofya linki hii hapa chini.

https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/acsee/index.htm

Chapisha Maoni

0 Maoni