Nyota wa filamu wa Hollywood wajiandaa kwa mgomo

 

Makumi ya maelfu ya nyota wafilamu wa Hollywood wanajiandaa kugoma baada ya kutofautiana dakika za mwisho katika mazungumzo baina ya umoja wao na makampuni yanayorusha filamu.

Hata hivyo Chama cha Waigizaji Filamu (SAG-AFTRA) kimeafiki kuongezwa muda wa mazungumzo na studio kubwa.

Vyama vyote hivyo vya waigizaji wa filamu vimishindwa kukubaliana kuhusiana na mirahaba pamoja na matumizi ya akili bandia.

Tangu Alhamis, wanachama wa vyama vya waigizaji wa Hollywood wanatarajia kujiunga waandishi wa fialamu katika mgomo.

Chapisha Maoni

0 Maoni