Wizara ya Maliasili na Utalii imeibuka Kidedea kwenye
Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) Jijini Dar es Salaam na
kukabidhiwa tuzo na Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Mapinduzi, Mhe. Dkt.
Hussein Ally Mwinyi ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Maonesho
hayo.
Akielezea Tuzo hiyo ya Banda bora na mashuhuri category ya
Wizara na Taasisi, Mwenyekiti wa Maonesho ya Saba Saba Wizara ya Maliasili na
Utalii, Bw. Filex John, amesema ni Matokeo chanya ya Uongozi mzuri wa Wizara
hiyo pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Watumishi wa Wizara hiyo ya utoaji
huduma kwa Kiwango cha juu kwa wote waliofika kwenye Banda hilo.
Bw. John amewashukuru wadau na wananchi wote waliojitokeza
kupata huduma kwenye Banda hilo la Maliasili, pamoja na ushirikiano waliotoa
katika kuhakikisha Maonesho hayo yanakuwa na Mafanikio Makubwa.
Muonekano wa Tuzo hiyo ya Banda Bora na Mashuhuri kwa upande wa Wizara na Taasisi za Umma.
0 Maoni