Hali
ya hewa ya joto imetapakaa katika maeneo ya kusini mwa Ulaya na kaskazini-
magharibi mwa Afrika, huku ikitarajiwa kuvunja rekodi ya joto kali katika siku
zijazo.
Joto
hilo kali linatarajiwa kufikia kipimo cha nyuzi jito 40 katika baadhi ya maeneo
ya Hispania, Ufaransa, Ugiriki, Croatia pamoja na Uturuki.
Huko
Italia joto litaongezeka na kufikia nyuzi joto 48, ambapo hali ya hatari
imetangazwa kwenye miji 10 ikiwamo ya Roma, Bologna na Florence.
Siku
ya Jumanne. mwanaume mmoja aliyekwenye umri wa miaka 40 alianguka na kufa
kaskazini mwa Italia kutokana na joto kali.
0 Maoni