Akili Bandia (AI) kuanza kuwaondoa ma-DJ kwenye ajira

 

Je, umewahi kufikiri kuwa upo klabu, muziki unakita na taa za rangi mbalimbali zinawaka kukupandisha mzuka wa kusakata disco.

Lakini unapoangalia juu eneo la chumba cha DJ, huoni mtu kutokana na kuwa upo kwenye kizazi cha mziki ulipangiliwa na kuchanganywa kwa kutumia akili bandia (AI).

Teknolojia ya kuchanganya muziki inazidi kuimaraka na kumbi za klabu sasa zinapunguza bajeti ya ma-DJ, hali inayoibua wasiwasi katika sekta ya muziki wa dansi.

Hata hivyo swali linabaki ni kweli komputa inaweza kuondoa uhalisi wa muziki wa klabu unaowaunganisha DJ na wachezaji?

Chapisha Maoni

0 Maoni