Huenda baadhi ya wasaidizi wa kiongozi wa dhehebu tata la
Kilifi huko Kenya, Paul Mackenzie, bado hawajakamatwa baada ya kubainika kwa
miili mingine mipya ya watu iliyozikwa kwenye eneo la kanisa hilo la msitu wa
Shakahola.
Miili kadhaa ya watu imefukuliwa katika msitu huo wa
Shakahola wiki hii, ambapo inaonyesha dhahiri maiti za watu hao zimezikwa
katika siku za hivi karibuni, baada ya kufunga hadi kufa.
Chanzo kimoja kutoka kwa timu inayofukua miili ya waumini wa
kanisa hilo tata, amesema miili hiyo imezikwa muda wa mwezi mmoja uliopita,
wakati timu inayofukua miili ilipopumzika zoezi hilo kwa wiki mbili.
Makaburi hayo ya watu yalionekana kuwa ni mafupi na
yamefukiwa kwa juu juu, hali inayoashiria kwamba bado kuna wasaidizi wa
kiongozi wa kanisa hilo, wanaoendeleza imani potofu ya waumini kufuanga hadi
kufa ili kukutana na Mungu.
Siku ya jumanne, timu ya wafukuaji makaburi ya waumini
waliozikwa msitu wa Shakahola imefanikiwa kufukua miili 16, ikiwamo baadhi ya
miili ya watu ambayo inaonekana imezikwa katika siku za karibu.
Chanzo: Nation
0 Maoni