Rais Samia, Mayele wang’ara tuzo TFF

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk. Samia Suluhu Hassan amepewa tuzo ya heshima kwa mchango wake katika kuendeleza maendeleo ya michezo.


Tuzo hiyo imetolewa katika  hafla ya Tuzo za TFF  jijini Tanga wengine waliopewa tuzo ni 

Mshambuliaji wa Yanga SC Fiston Kalala Mayele ameshinda Tuzo ya Mchezaji bora (MVP) wa Msimu wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023 akiwashinda Saido Ntibazonkiza wa Simba SC,  Mzamiru Yassin (Simba SC), Bruno Gomes (Singida) na Djigui Diarra (Yanga SC).


Kiungo wa Simba SC Saido Ntibazonkiza Raia wa Burundi ameibuka Mshindi wa Tuzo ya Kiungo bora wa msimu wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023 akiwashinda Bruno Gomes (Singida), Aziz Ki (Yanga), Clatous Chama (Simba) na Mzamiru Yassin (Mzamiru Yassin).


Kwa upande wa ufungaji bora Mshambuliaji wa Young Africans SC, Fiston Mayele na kiungo wa Simba SC, Saidi Ntibazonkiza wametwaa tuzo hiyo, Ntibazonkiza na Mayele 

wametwaa tuzo hiyo baada ya kila mmoja kufunga magoli 17 kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu 2022/23.



Golikipa wa Yanga SC Djigui Diarra Raia wa Mali ameshinda Tuzo ya golikipa bora wa msimu wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023 akiwashinda Aishi Manula wa Simba SC na Benedict Hauli wa Singida


Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC Raia wa Burundi Saido Ntibazonkiza amshinda tuzo ya Fair Play (Uungwana michezoni)



Kocha wa Yanga SC Nassredine Nabi ameshinda tuzo ya Kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/23 akiwashinda Kocha Hans Van Pluijm (Singida) na Roberto Oliveira (Simba SC).

 

Kwa upande Kombe la ASFC Golikipa namba moja wa Yanga SC Djgui Diarra ametangazwa kuwa Mshindi wa tuzo za Golikipa bora wa michuano ya Kombe la ASFC.


Mwingine ni Mlinzi na Nahodha wa Young Africans SC, Bakari Nondo Mwamnyeto ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup) akiwashinda Clement Mzize (Yanga) Prince Dube (Azam FC) Abdul Sopu (Azam FC) na Fiston Mayele (Yanga SC.

Chapisha Maoni

0 Maoni