Trump kufikishwa Mahakamani Miami, Florida leo

  

Donald Trump amelala usiku Miami, Florida, kabla ya kufika Mahakamani hii leo kukabiliana na mashtaka ya kutohifadhi vyema nyaraka za siri za taifa.

Rais huyo wa zamani wa Marekani alitumia usafiri wa ndege kutoka kwenye klabu yake ya golfu ya Bedminster, New Jersey hadi hoteli yake ya Doral ya Miami.

Trump anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya kukaa kinyume na sheria na nyaraka za siri, zikiwemo baadhi za siri za nyuklia.

Hii ni mara ya pili katika mwaka huu kwa Trump kushitakiwa kwa uhalifu Mahakamani.

Chapisha Maoni

0 Maoni