Bibi 'aliyekufa' azinduka kwenye jeneza

 

Waombolezaji katika msiba wa bibi moja huko Ecoador, wamejikuta wakipatwa na mshangao kubaini kwamba marehemu yupo hai akiwa kwenye jeneza.

Bibi huyo Bella Montoya mwenye umri wa miaka 76, alithibitishwa na madaktari kuwa amekufa wiki iliyopita kufuatia kupatwa na kiharusi.

Baada ya saa tano alizinduka siku ya Ijumaa, wakati ndugu wakiandaa kumbadili nguo zake kabla ya kwenda kumzika na kumuona akihaha kupumua.

Bibi Montoya amerejeshwa hospitali katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), na tayari Waziri wa Afya wa Ecuador ameunda timu kuchunguza tukio hilo.


Chapisha Maoni

0 Maoni