Azimio kuhusu mkataba na DP World lapitishwa na Bunge

Bunge limepitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai, wenye lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo lililowasilishwa bungeni leo tarehe 10 Juni 2023 limepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.

Awali kabla ya wabunge kuchangia, Waziri wa Ujenzi na uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa alilielezea bunge kuhusu mkataba huo na manufaa yake kwa Taifa na kufafanua hoja zilizoibuliwa na wadau ikiwemo ya muda wa utekelezaji wake.

Kinyume na inavyosemwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii, Prof. Mbarawa amesema pamoja na uwekezaji utakaofanyika bandarini, suala la ulinzi litabaki mikononi mwa Serikali.

“Jukumu la ulinzi na usalama katika Bandari ya Dar es Salaam litaendela kusimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama,” alisema Prof. Mbarawa.

Chapisha Maoni

0 Maoni