Ajali ya ndege: Watoto wanne wakutwa hai msituni baada ya siku 40

Watoto wanne wamepatikana wakiwa hai, baada ya kunusurika katika ajali ya ndege na kukaa wiki kadhaa wakijilisha wenyewe, kwenye msitu wa Amazon huko Colombia.

Rais wa Colombia amesema oparesheni ya kuwaokoa watoto hao wenye umri wa miaka 13, minane, minne pamoja na wa mwaka mmoja, kuwa ni "furaha kwa taifa lote".

Mama wa watoto hao pamoja na marubani wawili, walikufa katika ajali hiyo ya ndege ndogo iliyoanguka msituni Mei mosi.

Oparesheni hiyo ya kuwatafuta watoto hao ilikuwa ni moja ya oparesheni kubwa iliyohusisha makumi ya wanajeshi na raia wa kawaida.

Chapisha Maoni

0 Maoni