Madaktari wamzuia Papa Francis kutoa baraka Jumapili

Madaktari wanaomtibu Papa Francis wamesema anaendelea kupona vizuri, baada ya kufanyiwa upasuaji, lakini wamemtaka kutotoa baraka za Jumapili akiwa kwenye kibaraza cha hospitali.

Papa Francis amefanyiwa upasuaji kwa muda wa saa tatu, kutibu henia ya tumboni kwenye hospitali ya Gemelli siku ya Jumatano.

Akiongea na waandishi wa habari leo, Daktari wa upasuaji Sergio Alfieri, amesema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 86, hatotoa baraka za wiki ili kuepusha kuathiri eneo alilopasuliwa.

Dk. Alfieri, ameongeza kwamba Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani, ataendelea kukaa hospitali kwa wiki yote ijayo.

Chapisha Maoni

0 Maoni