TANZIA! Benard Membe afariki dunia

 

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernad Membe amefariki dunia.



Membe ambaye pia alikuwa Mwanadiplomasia na Mtaalamu wa Masuala ya Mahusiano ya Kimataifa na Usalama na Mbunge kwa Miaka 15 amefariki Dunia akiwa anatibiwa katika hospitali ya Kairuki Dar es salaam.


Kwa mujibu wa taarifa awali zilizotolewa na kituo cha Itv Tanzania zinasema Membe alipata changamoto ya kifua na alfajiri ya leo na baadae kupelekwa hospitalini hapo kwa matibabu.


Marehemu Membe alizaliwa  9 Mei 1953 na amefariki siku 3 baada ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake akiwa ametimiza miaka 70


Membe aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na mwaka 2020 aliwania urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo baada ya kutimuliwa CCM wakati wa utawala wa hayati John Magufuli 


Kesi yake na Cyprian Musiba March 28 

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuamuru mwanahabari anayejitambulisha kama mwanaharakati huru, Cyprian Musiba kumlipa fidia ya shilingi bilioni 6 aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe.

Katika hukumu na Jaji Joacquine De Mello aliyeisikiliza kesi hiyo Musiba alitakiwa ametakiwa kumlipa Membe kiasi hicho cha fedha pamoja na gharama zote za uendeshaji wa kesi kwa zaidi ya miaka miwili.

Pia imeweka zuio la kudumu kwa Musiba la kutokumkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake.




Chapisha Maoni

0 Maoni