Rais Samia amlilia Membe aandika ujumbe mzito

Rais Dk Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri wa mambo ya nje na kada wa CCM Benard Membe.

Rais Samia katika ukurasa wake kwenye mtandao wa twita ameandika “Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndugu Bernard Membe”


Rais Samia amesema Kwa zaidi ya miaka 40, Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyeitumikia nchi  kwa weledi. “Pole kwa familia, ndugu, jamaa & marafiki. Mungu amweke mahali pema. Amina.”



Membe alizaliwa  Novemba 9  1953 alishika  kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na mwaka 2020 aliwania urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo baada ya kutimuliwa CCM wakati wa utawala wa hayati John Magufuli na kurejea tena katika utawala wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Chapisha Maoni

0 Maoni