Tanzania yachaguliwa kuwa makao makuu ya baraza la michezo Afrika


 Tanzania imechaguliwa kuwa makao makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya nne Afrika.

Ushindi huo umepatikana baada ya nchi Wanachama wa baraza hilo linaloundwa na nchi 14 kuichagua kwa kura. 


Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika leo Mei 4, 2023 jijini Arusha Tanzania ikiwa miongoni mwao.



 Kinachofuata baada ya kuwa wenyeni ni kusaini mkataba wa makubaliano ya kuwa wenyeji, kuratibu kwa miaka miwili ya mwanzo watumishi wakiwemo katibu mkuu na maofisa wa mipango watatoka nchini.


Makao makuu ya baraza hilo ni nchini Cameroon.


Chapisha Maoni

0 Maoni