Sababu za vifo wavuvi watatu Geita zatajwa


 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita limetaja sababu za wavuvi  watatu kufariki wanaojishughulisha na uvuvi ndani ya Ziwa Victoria kufariki dunia.

Wambura Fidel ni ofisa mkaguzi wa jeshi hilo amesema ajali hiyo ilitokea usiku wa jumatatu na kuwa sababu ya kuzama kwa mtumbwi uliokuwa ukitumiwa na wavuvi hao ulianza kuvuja na kuingiza maji na baadae kuzama.


Amesema mtumbwi huo ulikuwa na watu sita ambao waliingia majini kwa ajili ya kufanya shughuli zao za uvuvi


“Walikuwa wakipambana kuchota maji kuyamwaga lakini kasi ya maji iliyokuwa inaingia ilikuwa ni kubwa, ikilinganisha na kasi ya maji ambayo wao walikuwa wanatoa,wananchi waliokuwa karibu na ene la tukio waliokoa watu watatu baada ya kusikia kelele za kuomba msaada na juhudi za kutafuta wengine watatu ziliendelea na walipatikana wakiwa wamekufa”


Wambura amewataja waliofariki kuwa David Mariatabu Mzula (25), Kamuli Mgogoro (20) na Faustine Cleophace Chibuga (28) wote ni wakazi wa kijiji cha Nungwe wilayani Geita na Walionusurika Kulwa Thomas (30), Dickson Alphonce (47) na Dickson Majura (22).

 

Chapisha Maoni

1 Maoni

Bila jina alisema…
Poleni jamani ila maji sio kitu ya mchezomchezo