RC Chalamila atinga na kibajaj aanza na TRA mgomo Kariakoo

 

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametaja utumiaji wa wafanyakazi wanafunzi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwa ndiyo chanzo cha migogoro na wafanyabiashara.



Chalamila amebainisha hayo katika ziara yake katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo ikiwemo soko la Mwenge ili kuangalia athari iliyosababishwa na mgomo wa wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo.



Amesema watendaji hao wa mamlaka kutokana na uchanga katika kazi inasemekana wana uwezo mdogo wa kuweza kutoa huduma stahiki kwa mteja.


Katika ziara hiyo amesema, ingawa hajaingia ofisini ametamani kujua mtaani watu wanasema nini, maeneo mengi aliyopita kinacholalamikiwa hasa ni kero zihusuzo kodi na utoaji wa risiti za kielektroniki.



Ametaja  eneo lingine  kuwa ni idara ya forodha ambayo imeweka viwango vikubwa vya kodi hasa kwa vitenge pamoja na ufuatiliaji kuwa mkubwa jambo linalokwamisha biashara zao.


 “Hii inamaana ya ufuatiliaji wa wateja wote waliolipa kodi bandarini, lakini jambo lingine ni kuwepo kwa kamata kamata kwa wafanyabiashara Kariakoo na kuwakosesha uhuru na kuwasumbua wateja hasa wanaotoka nchi za Congo, Zambia na nyinginez”, amesema.


Ziara ya ghafla mtaani ya Chalamila inafanyika ikiwa ni siku moja tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipomhamisha kutoka mkoani Kagera.

Chapisha Maoni

0 Maoni