Profesa Jay ajitokeza kwa mara ya kwanza atoa waraka mzito


Msanii maarufu wa bongofleva  na aliyewahi kuwa mbunge wa Mikumi nchini  Tanzania Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay amejitokeza kwa mara ya kwanza  kwenye mitandao ya kijamii na kueleza  mazito.


Prof Jay amejitokeza kupitia mtandao wa instagram na kuandika waraka mrefu ikiwa zimepita siku zaidi  ya 4 za kutoandika chochote kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii baada ya kuugua na kulazwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili.



Katika mtandao huo Profesa Jay ameanza kwa kuandika "Salaam Ndugu zangu, kwanza namshukuru sana MUNGU aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai, hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu), 

kipekee namshukuru sana Mhe. Rais Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi, Asante sana Mama pamoja na Serikali yako yote kwani Viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji"



"Tatu namshukuru sana Mwenyekiti wa Chama changu cha CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe, Wanachama na Viongozi wote waandamizi wa Chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na Serikali, zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa Muhimbili kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu AHSANTENI SANA"


Mkali huyu wa Bongofleva pia alimalizia kwa kuwashukuru Watanzania wote waliojitolea kwa maombi na pesa ambazo zilimsaidia sana kulipia gharama za awali kabla ya Serikali kuingilia kati na kusema itagharamia kila kitu.

Aidha waraka huo umeshukuru Watanzania vikiwemo  Vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii Watumishi wa Mungu kama Wachungaji, Mashekh na Mapadre walioshiriki kunusuru afya yake.

Mwisho akaishukiru familia yake akiwemo Mke wake, Kaka zake, Dada zake, Wadogo zake na Familia yote ya Mzee Haule.


"Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana Mungu ni mwema sana siku zote a

,Ahsanteni…… Joseph Haule (Prof. Jay)


Chapisha Maoni

0 Maoni