Wachungaji wawili watata Kenya kupanda kizimbani

 


Wahubiri wawili wa mkoa wa Pwani wanaoshikiliwa na polisi kuhusiana na vifo vya waumini wao, wanatarajiwa kufikishwa kwenye mahakama ya Mombasa hii leo.

Wahubiri hao wa makanisa ya Good News International Mchungaji Paul Mackenzie na wa kanisa la New Life Prayer Centre Mchungaji Ezekiel Odero watafikishwa mahakama ya Shanzu.

Serikali ya Kenya inamhusisha Mackenzi na vifo vya watu huko Shakahola ambapo zaidi ya miili ya watu 110 ilikutwa.

Mchunguzi Mkuu wa Serikali wa matukio ya vifo Johansen Oduor, jana alisema baadhi ya watu waliokufa Shakahola walikufa kwa njaa na wengine walikufa kwa kukosa hewa.

Chapisha Maoni

0 Maoni