Mpalestina agoma kula hadi kufa gerezani Israel

  


Kiongozi wa juu wa wapiganaji wa kikundi cha Jihad Palestina, Khader Adnan, amakufa gerezani nchini Israeli baada ya mgomo wa kutokula wa siku 86.

Mamlaka ya Magereza ya Palestina imesema ilimkuta akiwa amepoteza fahamu leo asubuhi, na alipelekwa hospitali lakini jitihada za kuokoa maisha yake zilishindikana.

Magereza wamesema Khader Adnan alikataa kufanyiwa vipimo vya kitabibu na kutibiwa hospitalini.

Baada ya kutangazwa kifo chake, wapiganaji wa Palestina walirusha makombora matatu ya rekoti kutokea ukanda wa Gaza, hakuna aliyejeruhiwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni