Rais Samia aipongeza Yanga kutinga nusu fainali CAFCC

 


Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa kutinga nusu fainali CAFCC

Kupitia akaunti yake katika mtandao wa twitter Rais Samia ameandika “Pongezi kwa Klabu ya Yanga kwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup), na kila la kheri katika maandalizi mliyoanza sasa kwa mchezo ujao”



“Mmeandika historia jalili. Mmetuheshimisha sana. Hamasa yangu inaendelea, na sasa imeongezeka. Kaifanyeni kazi.” alisisitiza 


Chapisha Maoni

0 Maoni