Mapya yaibuka mauaji ya waziri wa kazi Uganda


Baada ya WAziri  wa Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda nchini Uganda, Charles Okello Engola kuuwawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake imeelezwa kuwa mlinzi huyo aliajiriwa muda mfupi.


Waziri huyo aliuwawa asubuhi hii akiwa nyumbani kwake Kyanja Kampala.Naibu msemaji wa polisi wa Kampala, Luke Owoyesigire amethibitisha.


Spika wa Bunge, Anita Among, ni miongoni mwa waliothibitisha kifo cha waziri huyo alipokuwa akiongoza kikao cha mashauriano alisema

“Leo asubuhi nimepata taarifa za kusikitisha kuwa Mh Engola amepigwa risasi na mlinzi wake na baadae kujipiga risasi. Roho yake ipumzike kwa amani,” Among alisema.


ILIVYOKUWA

Waziri Okello alikuwa anatoka nyumbani kwenda kazini ambapo ghafla Mlinzi wake alimpiga risasi kisha akaanza kupiga risasi juu huku akikimbiakimbia Mtaani, mashuhuda wameeleza Mlinzi huyo alisikika akisema hajalipwa mshahara kwa muda mrefu licha ya kufanya kazi na Waziri huyo.


Taarifa zaidi zinaeleza mlinzi huyo baadaye aliingia Saluni moja iliyopo Jirani na nyumba ya Waziri kisha akawataka waliokuwa ndani kutoka nje na akajifungia na kujipiga risasi na kufariki pia.

Chapisha Maoni

0 Maoni