Mamba wamuua Rais wa wafugaji wa mamba

 

Mkulima anayefuga mamba, ameshambuliwa na mamba wake kaskazini mwa Cambodia na mwili wake kuchanwa chanwa vipande na mamba wapatao 40, baada ya kuanguka kwenye banda lao.

Mkulima huyo Luan Nam, 72, alikuwa anajaribu kutoa kwenye banda yai lililokuwa limelaliwa na mamba, ndipo myama huyo alipoing’ata fimbo yake na kumvuta bandani.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mey Savry, amesema baada ya kudondoka bandani, mkulima huyo aliaanza kushambuliwa na mamba wengine aliokuwa anawafuga.

Savry ameliambia shirika la habari la AFP news, kwamba tukio hilo limetokea katika mji wa Siem Reap siku ya jana Ijumaa.

Mwili wa mkulima Nam ambaye alikuwa ni rais wa chama cha wafugaji wa mamba Cambodia, ulitolewa ukiwa na alama za kung’atwa, ambapo mkono wake mmoja haukupatikana.

Chapisha Maoni

0 Maoni