Rais Samia atoa somo kwa TAPSEA, TRAMPA

 

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka makatibu muhtasi na watunza kumbukumbu kuzingatia nidhamu na maadili ya kazi na kutunza siri.


Rais Samia ametoa wito huo kwenye kilele cha mkutano wa kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika Fumba Zanzibar.


Amewataka kufanya kazi kwa ufanisi na nidhamu katika ufanyaji wa kazi kwa kiwango kinachotakiwa “Ufanisi maana yake ni kuikamilisha kazi vile inavyotakiwa, kwa kiwango kinachotakiwa na wakati unaotakiwa. Ukiwa na nidhamu na uadilifu utazalisha kazi kwa wakati kwa kiwango kinachotakiwa na muda unaotakiwa,” amesema Rais Samia 


Akizungumzia alipotoka Rais Samia amesema “Anayekujua ndio anayekuthamini, asiyekujua hawezi kukuthamini, mimi nilianza kama muweka kumbukumbu, ni taasisi nayoijua ndiyo maana naithamini labda wenzangu hawa, walitoka shule nakwenda moja kwa moja nafasi za juu”.



Aidha, Rais Samia ametoa fedha ya mafuta kuwapeleka Kaskazini na Kusini mwa Visiwa vya Zanzibar makatibu mahsusi pamoja na watunza kumbukumbu na nyaraka ili waione Zanzibar.

Chapisha Maoni

0 Maoni