Vyura wa Kihansi kurejeshwa nchini kutoka Marekani Julai

 

Suala la vyura wa Kihansi limechukua sura mpya baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharage Chande kusema wataanza kurejeshwa vyura hao nchini Julai 2023.



Chande amebainisha  wakati wa mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam  amesema vyura wa Kihansi wanaohifadhiwa nchini Marekani ambao kwa sasa wamefikia zaidi ya 6000 wataanza kurejeshwa nchini baada ya kukamilika kwa mradi ambao uwepo wao ungeathiri ukuaji wao.



Chande amesema katika ujenzi wa miradi mikubwa huwa wanaweka mipango ya kuhifadhi ikolojia ambao mzunguko wake ni miaka 20 na kuwa vyura hao walihamishiwa nchini Marekani kutokana na Tanzania kutokuwa na maabara maalumu kwaajili ya kuwatunza.


Amesema vyura hao walitakiwa kurejeshwa 2021 ikiwa ni  mzunguko wa ikolojia miaka 20 lakini zoezi la kuwarejesha  lilikumbana na changamoto ya mlipuko wa  Uviko-19.


“Ili jambo la vyura wa Kihansi linashereheshwa  kama vile ni wrong decision vyura wale walikuwa wanakuwa kutokana na mvuke wa maporomoko ya  maji ya Kihansi kabla ya kujenga tulihakikisha ujenzi wetu hautawathiri na kuwapoteza kama walivyopotea kunguru wa mabaka meupe,” alisema Chande.


Chande amesema uamuzi wa kuwahifadhi vyura hao ulikuwa wa faida na kwamba katika kipindi chote walichohifadhiwa, nchi imepata faida “mradi wa Kihansi umezalisha zaidi shilingi trilioni 3 na ikolojia imelindwa”.


Tangu vyura 500 wapelekwe Marekani mpaka sasa, Tanesco imetumia zaidi ya Sh 900 milioni kuwatunza huku asilimia kubwa ya gharama zikitolewa kwa ufadhili wadau wa mazingira na wahifadhi.



Tangu mwaka 2000 mpaka June 2019, gharama za matunzo ya vyura hao zililipwa na Benki ya Dunia (WB) na Global Environment Facility ili kutoa fursa ya mradi wa umeme kutekelezwa.


Taarifa ya  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/2022 ilibainisha kuwa Vyura 500 bado wapo Marekani licha ya kumalizika kwa mkataba wa matunzo.


Ripoti ya CAG ilibainisha kuwa kwa miaka 22 (2000-2022), Tanzania imetumia TZS bilioni 6.69 kutunza vyura 500 iliowapeleka Marekani ili kuepuka hatari ya kupotea kutokana na utekelezaji mradi wa umeme wa Kihansi.


Serikali ilipeleka vyura hao katika bustani za Bronx na Toledo ili kupisha ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika Bwawa la Kihansi miaka 22 iliyopita kwa mkataba ulioisha mwaka 2020 na ikaongeza miaka miwili hadi mwaka 2022.


Chanzo:Tanesco/Mwananchi/Mimihabari



Chapisha Maoni

0 Maoni