Afungua mlango wa ndege ikitua ili apate hewa safi

 

Mwanaume mmoja amekamatwa kwa kufungua mlango wa ndege ya kampuni ya Asiana, wakati ndege hiyo ikielekea kutua kwenye uwanja wa ndege nchini Korea Kusini.

Abiria wote 194, waliokuwamo walinusurika kifo, baada ya ndege hiyo kutua salama huku mlango wake ukiwa wazi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Daegu, Ijumaa.

Baadhi ya abiria walipoteza fahamu wakati wengine wakipata changamoto ya kupumua na walikimbizwa hospitali kwa matibabu, shirika la Yunlop news limeripoti.

Imeripotiwa mwanaume huyo umri wake ni kati ya miaka 30, alisema kwamba alikuwa anahisi kuishiwa na hewa na kutaka kutoka haraka kwenye ndege.

Haya hivyo, Polisi wamedai kuwa katika mahojiano mwanaume huyo aliwaambia alikuwa anakabiliwa na msongo wa mawazo baada ya kupoteza ajira.

Chapisha Maoni

0 Maoni