EWURA yatangaza kushuka kwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza  bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini kuanzia May 5.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi mkuu EWURA Dk James Mwainyekule kwa vyombo vya habari imesema bei hizo zimezingatia bei za rejareja za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa Shilingi 187/Lita, Shilingi 284/Lita na Shilingi 169/Lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la tarehe 1 Machi 2023.



Kwa Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara), bei za rejareja za Aprili 2023 kwa mafuta ya petroli na dizeli zimepungua kwa Shilingi 158/Lita na Shilingi 231/Lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la tarehe 1 Machi 2023. 


Kutokana na kuisha kwa mafuta ya taa kwenye matanki ya kuhifadhia yaliyopo Tanga, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.


Kwa upande wa  mikoa  ya Kusini (Mtwara, Lindi, and Ruvuma), bei za rejareja za Aprili 2023 kwa mafuta ya petroli na dizeli zimepungua kwa Shilingi 220/Lita na Shilingi 176/Lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la tarehe 1 Machi 2023.





Chapisha Maoni

0 Maoni