Dk Mpango awaonya mawakili vishoka wasio na maadili

 

Makamu  wa Rais, Dk Philip Mpango ametoa wito kwa Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Kamati ya Mawakili kuchukua hatua kali za kinidhamu na kisheria dhidi ya mawakili wote wanaoharibu heshima ya taaluma ya sheria kwa kukosa uadilifu na maadili mema.

 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa TLS uliofanyika jijini  Arusha , Dk Mpango amesema Kumekuwa na tuhuma za baadhi ya mawakili kujihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu kwa maslahi yao binafsi ikiwemo kuwasaliti wateja kwa kupokea rushwa kutoka upande wa pili.

 

Aidha, ameitaka  TLS kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kutoa elimu kwa umma kuhusu suala la mihuri ya kielektroniki ili kuondokana na suala la vishoka na mawakili wanaotumia mihuri isiyo halali kufanya kazi za uwakili.

 


 Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro ametoa wito kwa wanachama wa TLS kushiriki kikamilifu katika mchakato wa katiba mpya pamoja na mchakato wa mabadiliko ya sheria zinazohusiana na siasa, uchaguzi na demokrasia ikiwa ni pamoja na ziendelee kuchambua, kubaini na kutoa mapendekezo ya sheria zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho au kuandikwa upya.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni