Waliokufa kwa kufunga Kenya wafikia 150

 


Miili zaidi mitano imefukuliwa leo Alhamis, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi katika eneo la dhehebu tata la Mchungaji Paul Mackenzie aliyeagiza waumini wake wafunge hadi kufa ili wakutane na Yesu.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Rhoda Onyancha, amesema miili iliyofukuliwa hadi sasa imefikia 150, na kuongeza kuwa leo ndio wamefukua idadi ndogo ya miili ikilinganishwa na siku za nyuma.

Onyancha ameeleza kuwa wanaume wawili watu wazima wameokolewa leo, wote hali zao ni nzuri, na kufanya idadi ya waliookolewa kufikia watu 72.

Ameongeza kuwa idadi ya watu walioripotiwa kupotea inaendelea kuongezeka na kufikia watu 594 hadi kufikia leo Alhamis na idadi ya miili iliyochukuliwa kipimo cha DNA imefikia 93.

Waumini wengine 14 kanisa hilo lililopo eneo la Shakahola nchini Kenya wameunganishwa na familia zao.

Chapisha Maoni

0 Maoni