Waliokufa mapigano ya Sudan wazidi watu 400

 

Machafuko ya nchini Sudan yameingia wiki ya pili wakati jeshi la nchi hiyo likipigana na vikosi vya Rapid Support Forces.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema zaidi ya watu 400 wamekufa, lakini takwimu halisi za vifo zinaweza kuwa juu ya idadi hiyo.

Hospitali nyingi zimefungwa na huduma za maji na umeme zimetatizwa, hali inayoashiria uwezekano wa kuibuka kwa mgogoro mkubwa wa kibinadamu.

Maujia ya wafanyakazi mashirika ya misaada wakiwamo watatu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, yamepelekea Mashirika ya Umoja wa Mataifa kusitisha shughuli zake Sudan.

Maelefu ya raia wa kigeni na wanadiplomasia wameondolewa Sudan mwishoni mwa wiki, huku zoezi la kuwaondoa wageni zaidi kwa ndege likiendelea leo.

Chanzo: BBC


Chapisha Maoni

0 Maoni