Amuua mkewe na kumtumbukiza kwenye sanduku

 


Wapelelezi wa kituo cha polisi cha Ruiru nchini Kenya wameshtushwa na maelezo ya mtuhumiwa anayedaiwa kumuua mkewe na kuuweka mwili wake kwenye sanduku na kisha kuutupa.

Katika maelezo yake ya kukiri kufanya mauaji aliyoyatoa Aprili 22, mtuhumiwa Morris Njuguna, 28, amesema alimuua mkewe usiku wa Aprili 18, katika makazi ya Mitikenda nje ya mji wa Ruiru.

Mkewe aitaye Risper Ndunge alikuwa na wakati mzuri Jumatatu ya wiki iliyopita katika moja ya hoteli ya mji huo ambayo yeye na mumewe Njuguna walikuwa wanafanya kazi pamoja.

Njuguna alikuwa ni mpishi katika hoteli hiyo iliyopo Ruiru, wakati mkewe waliodumu naye kwa miezi tisa alikuwa akifanya kazi kama Keshia.

Wanandoa hao penzi lao lilichipua katika eneo linalouzwa samaki ambalo walikuwa wakikutana na baadaye Njuguna alimuombea kazi ya ukeshia Ndunge katika hoteli anayofanya na kupata.

Wakati wakihudumia wateja siku ya Jumatatu, hakuna ishara yoyote iliyoashiria kwamba Ndunge angeuawa na mumewe huyo.

Wakiwa nyumbani ndipo ugomvi wa mali ulipoibuka na Njuguna akamshika mkewe Ndunge na kumbamiza ukutani na kichwa chake kugonga ukuta na kupoteza maisha papo hapo.

Kifo cha mkewe kilimshtua Njuguna na kuamua kuuingiza mwili wake kwenye sanduku na kulitumbukiza kwenye kiroba cheupe na kuutupa ili kuepuka kukamatwa.

Hata hivyo, mwili wa mkewe ulibainika siku inayofuata ukiwa kwenye kiroba mita 500 kutoka nyumba yao waliuokuwa wamepanga wanandoa hao.

Njuguna alikamatwa Aprili 21. Majirani zake wa makazi ya Mitikenda wameeleza walimuona Njuguna akihangaika kubeba kiroba hicho.

Chanzo: Nation Media

Chapisha Maoni

0 Maoni