SIMANZI! Baba auwa watoto wake wawili kwa sumu kisa kizima kiko hapa

SIMANZI 

Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia na mmoja kunusurika kifo baada ya kudaiwa kulishwa sumu na baba yao mzazi.

TAZAMA VIDEO

Tukio hilo limetokea katika eneo la Kwangwale Chanika Ilala Jijinj Dar es Salaam kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia baina Karim Chamwande na mke wake.


MWENYEKITI AFUNGUKA

Mwenyekiti wa mtaa huo Bakari Seif amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea tarehe 23 mwezi April majira ya saa 10 usiku wa kuamkia Idd Pili baada ya majirani kushtuka kuwepo na tukio hilo.


Seif akihojiwa na mwandishi wa TBC1 alisema kuwa alipopata taarifa alifika kuwaokoa watoto wakiwa na vyombo ulinzi waliwapeleka watoto hospitali ya Nguvukazi ambapo mtoto mdogo alifariki wakiwa njiani.


Akisimulia tukio hilo Mohamed Ibrahimu ni jirani na nyumba ilipotokea tukio hilo anasema kuwa alipofika karibu na choo cha nyumba hiyo alisikia mtu akiwa kama anavunja miti ndio aliposogea na kuhamaki kumuona mtoto ambaye alimuokoa na kwenda kutoa taarifa kuwa amejiua.


Ibrahimu anaeleza kuwa watoto hao watatu walikuwa wakiishi na mama wa mzazi wa mtuhumiwa Karimu ambaye yeye alikuwa akiishi peke yake baada ya kutengana na mkewe katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Chanzo:TBC1



Chapisha Maoni

0 Maoni