SIMANZI! Vifo Wanafamilia Wanne, Daktari Aeleza Siri Nzito

 

Baada ya taarifa ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuthibitisha vifo vya watu wanne baada ya kuvuta hewa chafu ya moshi kutoka kwenye jenereta madaktari wafafanua.


TUKIO LENYEWE 

Katika tukio hilo lililotokea siku ya Jumatano Aprili 19, 2023 maeneo ya Chang’ombe wilayani Temeke, Jijini Dar es Salaam lilisababisha vifo vya wanafamilia ambao wanadaiwa usiku familia hiyo iliwasha jenereta baada ya umeme kuzimika na kuliweka ndani ya nyumba.


TAARIFA YA POLISI

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro alisema kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo. 


Kamanda Muliro aliwataja waliofariki kuwa ni Kazija Mohamed (21), Munir Ibrahim (7), Munira Ibrahim (6) Muyyat Ibrahim (3).

huku  mume Ibrahim Juma (28) na mke na Aisha Ayubu (29) wapo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiendelea na matibabu.


DAKTARI  AFUNGUKA

Kutokana na tukio hilo tahadhari zimetolewa na wataalam wa afya na kinga za majanga wakiwemo madaktari ambapo kwa upande wake Dk Joseph Kimaro alisema kuwa kilichosababisha vifo hivyo ni kutokana na kuvuta hewa ya ukaa kutoka katika jenereta lililowashwa ambayo huathiri mfumo mzima wa upumuaji na hata kuzuia upatikanaji wa hewa ya oxygen.


Dk Kimaro katika mahojiano yake na Kipindi cha Goodmorning alisema baada ya mtu kuvuta carbon monoxide madhara huanza kutokea ambapo muathirika huhisi maumivu ya kichwa kwa mbali na mwili kuanza kuchoka, kichefuchefu pamoja na hali ya kutapika. 


Alisisitiza kuwa kiwango cha Monoxide kinapozidi mwilini na kufikia 7.4 ataanza kupoteza fahamu na kama hatopata msaada wa haraka basi atapoteza maisha.


HUDUMA YA KWANZA 

Kwa mujibu wa Dk Kimaro alisema mtu aliyeathiriwa na hewa hiyo anaweza kuhudumiwa kwa kumtoa katika eneo alilopo na kuwasiliana na hospitali iliyopo karibu ambapo ataongezewa oxygen kwa kiwango cha juu na matibabu mengine ili kuweza kuokoa uhai wake.


ATOA TAHADHARI 

Ambapo alisisitiza kuwa matukio hayo yamekuwa yakitokea lakini wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari za haraka haswa wanapotumia majiko ya mkaa ikiwemo kuhakikisha katika eneo husika kuna hewa inayoingia na kutoka. 


Aidha alisisitiza kutolala na majiko ya mkaa ndani ya nyumba kwani huzalisha hewa yenye sumu ya carbonmonoxide zikiwemo pia heater zinazotumia gesi kwani nazo hupunguza kiwango cha oxygen ndani ya nyumba.



VYOMBO VYA MOTO

Suala ambalo limezoeleka bila kujua athari zake ni pamoja na kuwasha vyombo vya moto katika garage za nyumbani kwani moshi wake huzalisha hewa ya ukaa ambayo ina athari kubwa kwa binadamu na viumbe hai wengine.


KUCHOMA DAWA ZA MBU

Akizungumzia suala hilo Dk Kimaro amesema suala hilo halijawa na utafiti unaoeleza madhara hasi kwa binadamu licha ya kutahadharisha wale wanaofunga pazia na milango huku wakiendelea na shughuli nyingine ndani ya nyumba, na kuwa madhara yake yanatofautiana kulingana na chanzo cha dawa husika. 

Chanzo: Tanpoltz/Wasafi/Mwananchi/Pichamtandao

Chapisha Maoni

0 Maoni