MUFT ZUBEIR! EID NI JUMAMOSI

 

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesema Sikukuu ya Eid el-Fitr itakuwa Jumamosi ya Aprili 22, 2023.


Mufti alitoa taarifa hiyo  Alhamisi, Aprili 20, 2023, Mufti Zubeir amesema, “kutokana na vyanzo vyetu na watu tunaoshirikiana nao kama Kenya, Zanzibar mwezi haujaonekana na tumethibitisha hilo, hivyo kesho tunaendelea kufunga siku 30 za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.”


Sikukuu hiyo Kitaifa itafanyikia jijini Dar es Salaam ambapo Swala ya Eid itaswaliwa Msikiti wa Mfalme Mohamed VI Bakwata Makao Makuu, Kinondoni kuanzia saa 1:30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuanzia saa 8:30 mchana.

Katika Baraza hilo, inatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Chapisha Maoni

0 Maoni