Ndege ya Russia yashambulia kimakosa mkoa wake

 

Wizara ya Ulinzi ya Russia, imesema kwamba ndege yake ya kivita imeshambulia kimakosa mji wa nchi hiyo wa Belgorod unaopakana na nchi ya Ukraine.

Gavana wa mkoa Vyacheslav Gladkov amesema shambulizi hilo la bomu limeacha shimo kubwa lenye upana wa mita 20 kati kati ya mji huo.

Watu watatu wamejeruhiwa na majengo kadhaa yameharibika, amesema Gavana Gladkov na kuogeza kuwa watu wamehamishwa katika moja ya ghorofa la makazi.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kwamba shambulizi hilo la makosa katika ardhi yao limefanywa na ndege ya kurusha makombora auna ya Su-34.

CHANZO: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni