Man United yatolewa nje michuano ya Europa

 

Timu ya Manchester United imeondolewa katika michuano ya ligi ya Europa baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Sevilla.

Katika mchezo huo kipa David de Gea na Harry Maguire waliigharimu Manchester United kwa makosa yao yaliyoisaidia Sevilla kuibuka na ushindi.

Kipigo hicho kimempa funzo kocha Mdachi Erik Ten Hag na kumuamsha kujua sasa anahitaji kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wenye uwezo.

Huku ikibabiliwa na mchezo wa nusu fainali ya FA dhidi ya Brighton jumamosi, wachezaji wa Manchester United wanahitaji kupona haraka ili kushinda mchezo huo.

Chapisha Maoni

0 Maoni