Afungwa jela miaka 25 kwa kukosoa vita ya Ukraine

 

Mwanaharakati mpinzani Vladimir Kara-Murza amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela nchini Russia kwa kuhusishwa na kukosoa vita ya Ukraine.

Kara-Murza alitiwa hatiani kwa uhaini na kusambaza taarifa za uongo kuhusiana na jeshi la Russia na kujihusisha na taasisi isiyofaa.

Mwanaharakati huyo raia wa Russia na Uingereza ambaye ni mwandishi na mwanasiasa ni miongoni mwa wakosoaji wa rais Putin waliokamatwa ama kulazimishwa kukimbia nchi.

Mwanaharakati mpinzani Vladimir Kara-Murza alikanusha mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili.

Wiki iliyopita alisema katika taarifa yake kuwa “Anasimamia maneno yote aliyoyasema..Na kwamba si tu hajutii bali anajivunia kwa yote”.

Chapisha Maoni

0 Maoni