Watumishi Ngorongoro wapigwa msasa utekelezaji wa masuala ya haki jinai

Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) kupitia Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu inaendesha mafunzo ya siku 5 kwa Askari wa Jeshi la uhifadhi kwa lengo la kuongeza ujuzi katika masuala ya haki jinai ambayo yanagusa utekelezaji wa majukumu ya ulinzi wa rasilimali za Wanyamapori, malikale na misitu.

Mafunzo hayo ambayo yanayotolewa na wataalam mbalimbali yamejikita kwenye mada  zinazohusu Haki jinai, Afya ya akili, Itifaki, uwekezaji, uongozi na nidhamu kwa watumishi yanafanyika kuanzia tarehe 31 Agosti hadi 4 Septemba 2026 Jijini Mwanza.

Akifungua mafunzo hayo mshauri wa Jeshi la Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro Kanali Fikiri Machibya amewataka askari hao kufanya kazi kwa kuzingatia nidhamu na utu kwa kila raia.

Kanali Machibya amesema askari wa uhifadhi wana jukumu la kulinda rasilimali za nchi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni.

Kadhalika, mafunzo hayo pia yamelenga kuwapa nafasi watumishi kubadilisha mazingira ya kazi ili kujenga hamasa ya uwajibikaji na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.




Chapisha Maoni

0 Maoni