Bodi ya
Wakurugenzi Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ikiongozwa na makamu
Mwenyekiti Dkt. Harriet Mtae jana tarehe 11 julai, 2026 imekagua uboreshaji wa
miundombinu ya utalii eneo la Nyayo za Laetoli lililopo hifadhi ya Ngorongoro.
Wakiwa
Laetoli Wakurugenzi hao wamekagua uhifadhi wa Nyayo zilizogundulika katika eneo
hilo miaka zaidi ya milioni 3.6 iliyopita na kuangalia hatua za utekelezaji wa
mradi wa Geopark unaohusisha ujenzi wa jengo la kupokelea wageni, jengo la
kupumzika wageni, jengo lililojengwa kwa ajili ya kuhifadhi Nyayo sambamba na
miundombinu mingine.
Naibu
Kamishna wa Uhifadhi Joas Makwati anayesimamia uhifadhi, utalii na maendeleo ya
jamii ameeleza kuwa ziara hiyo imelenga kutathmini utekelezaji wa miradi
inayofanywa na mamlaka kwa lengo la kuimarisha shughuli za uhifadhi, kuboresha
huduma za utalii na kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Hifadhi ya
Ngorongoro.
Pamoja na
kukagua miundombinu ya utalii wakurugenzi hao wamepokea taarifa ya hatua
zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na mipango ya kuendelea
kuboresha mazingira ya utalii na shughuli za uhifadhi.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya NCAA, Dkt. Harieth Mtae, alisema miradi hiyo inaakisi
dhamira ya mamlaka ya kuendelea kuwekeza katika uboreshaji wa vivutio vya utalii
na kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa wageni.
Ameongeza
kuwa maboresho hayo yanatarajiwa kuongeza thamani ya vivutio vya utalii,
kuvutia watalii zaidi na kuendelea kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kama moja
ya vivutio vinavyoongoza duniani.


.jpeg)
0 Maoni