Jacob Lekumbere,Afisa Utalii kutoka
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro hatosahau siku alipotumia mbinu za
kimedani kumkwepa simba aliyetazamana naye uso kwa uso.
Jacob
akiwa ndani ya hifadhi ya Ngorongoro,hifadhi iliyojaa kila aina ya
wanyama siku hiyo aliamka asubuhi kuelekea kwenye majukumu
yake.
Akiwa porini alikutana na pundamilia,alipowaangalia wale
pundamilia walikuwa wamekaa mkao wa tahadhari,Jacob machale naye
yakamcheza akaanza kutembea kwa tahadhari.
Mara paaa, kutupa
jicho umbali wa mita tatu simba jike yupo mbele yake,alichofanya
Jacob ni kumuangalia usoni simba yule,wote wawili wakawa
wanaangaliana.
Jacob alimuangalia simba na simba naye
alimuangalia Jacob,Jacob alipomuona simba hachezeshi masikio wala
mkia akajua simba hajakasirika.
Kilichofuata Jacob akawa kila
baada ya sekunde kadhaa anarudi nyuma kidogo kidogo mpaka akafika
umbali wa mita 40 huku simba akiwa amesimama anatafakari la
kufanya,hatimaye Jacob akajiokoa.
Karibu Ngorongoro uone
maajabu

0 Maoni