Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Ndugu Asha-Rose Migiro, leo Ijumaa Juni 5,2026 amefanya
mazungumzo na Mheshimiwa Marianne Young, Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania, katika Makao Makuu ya CCM, Dodoma.
Mazungumzo hayo
yalihusu maeneo ya ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na
Uingereza, kwa kuzingatia vipaumbele vilivyobainishwa katika Ilani ya
CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2025–2030, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Viongozi hao
walijadili fursa za kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya
kijamii na kiuchumi, hususan katika kuwawezesha vijana na wanawake
kupitia elimu, ujuzi, ubunifu na uwekezaji.
CCM inaendelea
kuthamini ushirikiano wa kimataifa unaochangia maendeleo endelevu na
ustawi wa wananchi wa Tanzania.



.jpeg)
0 Maoni