Katika bajeti ya Wizara ya
Maliasili na Utalii, makabila ya Wadatoga na Wahadzabe ambayo ni
sehemu ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai walitia nakshi na uturi bajeti
hiyo kwa kumsindikiza waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu
Kijaji (Mb) kuingia katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.
Wadatoga
ni waumini wa kuoa mke zaidi ya mmoja wanaotokana na jamii yao, wana
uwezo wa kuoa hadi wake kumi na kila mke akafurahia utamu wa ndoa
kutoka kwa mume wake.
Kwa Jamii hii kuwa na wake wengi si
heshima tu bali unachukuliwa kama uchumi kwa kuwa utapata watoto
wengi watakaokusaidia shughuli za kuchunga mifugo, kulima chakula cha
familia, kufanya kazi za uhunzi, kujenga maboma ya familia na kutanua
ukubwa wa jina la ukoo.
Wadatoga hawaishiwi "Power"
kwasababu hawali chipsi mayai, soseji wala Baga, hawatafuti energy
wala dawa za Congo,hawana mawazo ya vikoba,ni mwendo wa vyakula vya
asili tu kama Ugali, mtama, ulezi, Maharage, mbaazi, viazi vitamu na
Maziwa ambapo mafuta ya kupikia hawanunui dukani bali yanatokana na
samli kutoka kwenye maziwa ya ng'ombe yaliyogandishwa kisha
kuchekechwa kwenye kibuyu maalum na kuzalisha mafuta ambayo
husafishwa kiasili na kukaa muda mrefu bila kuharibika.
Kama
wewe ni kijana na unataka kuwa na uwezo wa kuwa na wake wengi karibu
makumbusho ya Urithi Jiopaki ujue siri ya wadatoga na vyakula vyao
vya miaka na mikaka.

0 Maoni